Magavana watakiwa kukoma kuwafuta wafanyikazi wa kaunti kiholela

Mwenyekiti wa Muungano wa wafanyikazi kwenye serikali za  kaunti nchini Roba Duba amewataka magavana wapya waliyoingia mamlakani kukoma kuwafuta wafanyikazi wa zamani kwenye kaunti hizo kwa kisingizio cha kuwa  wafanyikazi hewa.

Akizungumza kwenye kikao na wanahabari mjini Mombasa Duba amesema kuwa muunganao huo kamwe  hautasita kuelekea  mahakamani kupinga maagizo ya kufutwa kiholela kwa wafanyikazi wa zamani waliyoandikwa na serikali za kaunti zilizotangulia.

Aidha Duba Amewarai magavana wapya waliyoingia mamlakani kuharakisha mchakato wa kutekeleza mikataba ya maelewano kwa wafanyikazi maarufu kama CBA ili kuangazia kikamilifu maslahi yao, akiongezea  kuwa magavana wengi wangali kuangazia mipangilio ya mishahara kama inavyohitahitajika kisheria..

Waakati huo huo amempongeza rais William Ruto kwa  kutwaa hatamu za kuongoza nchi huku akimrai kuangazi maswala ya  pensheni kwa wafanyikazi kikamilifu  kwa kutoa maagizo ya ukaguzi wa mashirika yanayosimamia fedha hizo.

Vile vile amemtaka rais Ruto kuishinikiza tume ya  SRC kutathmini upya mishahara ya wafanyikazi wa serikali za kaunti nchini kufuatia kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini.

Mwenyekiti huyo vilevile ameyakashifu mashirika  ya serikali yanayosimamia pensheni akisema kuwa hayajakuwa yakitekeleza majukumu yao ipasavyo na kwamba  kwa kiasi kikubwa  yameshiriki kuhujumu haki za wafanyikazi wa serikali za kaunti nchini.

.

https://phicmune.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287