ABDULSWAMAD AAPISHWA RASMI KUWA GAVANA WA MOMBASA

Hatimaye aliyekuwa mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameapishwa rasmi kuwa gavana mpya wa kaunti ya Mombasa kwenye sherehe aliyoandaliwa katika bustani ya Mama Ngina Water Front Mjini Mombasa.
Abdulswamad ambaye anachukua hatamu ya kuwa gavana wa pili wa kaunti hiyo,amewashukuru wakaazi wa Mombasa kwa kumpa nafasi ya kuwaongoza huku akiahidi kuwahudumia wote bila ya kuwabagua.
Wakati huo huo Nassir amewarai waliyokuwa wapinzani wake kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha ugavana kuweka kando tofauti zao za kisiasa kushirikiana naye katika safari ya kuiendeleza na kuibadilisha kaunti ya Mombasa kimaendeleo.
Hatahivyo akiwahutubia mamia ya wakaazi walijitokeza kushuhudia sherehe ya kuapishwa kwake, Nassir ameahidi kuwa uongozi wake utafanikisha Ugatuzi ipasavyo kwenye kaunti hiyo ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na kutengeneza fursa za ajira kwa wakaazi.
Aidha Nassir amesema kuwa ndani ya siku mia moja za utawala wake atahakikisha kuwa huduma za serikali ya kaunti ya Mombasa zitapatikana kwa njia raisi kupitia mpango Huduma Mtaani ambao utabadilisha mchakato mzima wa kutafuta huduma kwenye kaunti hiyo.
Katika sekta ya afya Abdulswamad amebainisha kuwa serikali yake itaanzisha mpango wa afya care unaonuia kuwawezesha wakaazi kutoka familia maskini kwenye kaunti hiyo kupata huduma za matibabu wakati wanapokuwa wagonjwa.
wakati huo huo akisema kuwa watatoa nafasi za mafunzo kwa madaktari ilikuwawezsha kutoa huduma za kiwango cha juu.
Vile Vile Katika Sekta ya elimu amesema kuwa serikali yake itaweka mpango wa basari utakaowawezesha wanafunzi kusoma bila kufukuzwa shule kwa sababu ya karo. Mpango huo uliopewa jina la Elimu Fund unatarajiwa kuwawezesha wanafunzi kutoka familia maskini kuendeleza masomo bila tashwishi.
Aidha Nassir amewahakikisha wakaazi wa kaunti ya hiyo kuwa utawala wale utashughulikia tatizo la mrundiko wa taka kwenye kaunti hiyo akisema kuwa ndani ya siku mia moja za utawala wake wanatarajia kuanza zoezi la kuokota na kuchakata taka hizo ili kusafisha mazingira.
Miongoni mwa viongozi wa kuu wa n mrengo Azimio walijitokeza katika sherehe hiyo ni pamoja na Martha Karua pamoja na Kalonzo Musyoka.