Kalonzo kuhudhuria sherehe ya uapisho wa Abdulswamad

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Abdulswamad Shariff Nassir kuwa gavana mpya wa kaunti ya Mombasa hapo kesho

Kulingana vyanzo vya habari kutoka chama cha Wiper, Kalonzo anatarajiwa kuwasili Mombasa alasiri ya leo kwa ajili ya sherehe hiyo itakayoandaliwa  hapo kesho katika bustani ya Mama Ngina Water Front.

Hatahivyo leo  asubuhi gavana mteule wa kaunti ya Mombasa  Abdulswamad Shariff Nassir alizuru eneo hilo kutathmini maandalizi ya Kwa ajili ya siku hiyo ambapo aliwataka wakaazi wa Mombasa kujitokeza kwa wingi  na jumuika kwenye sherehe hiyo.

Itakumbukwa kuwa mnamo siku ya jumatatu mwenyekiti wa kamati ya kusimamia sherehe hiyo Joab Tumbo alidokeza kuwa wanatarajia zaidi wakaazi  2000 kuhudhuria sherehe hizo.

https://kukrosti.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287