Wakaazi Kinango wapata afueni ujenzi wa bwawa la kizingo ukiratajiwa kukamilika

Huenda tatizo la ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo kaunti ya Kwale likazikwa kwenye kaburi la sahau wakati ujenzi wa  bwawa la Kizingo utakapokamilishwa hivi karibuni.

Bwawa hilo lenye uwezo wa  kuhifadhi  lita milioni 5.1 za maji ni miongoni mwa miradi mikubwa iliyoanzishwa  na utawala wa aliyekuwa gavana wa kaunti  hiyo Salim Mvurya na ambao kwa sasa unatekelezwa na gavana mpya wa kaunti hiyo Fatuma Achani.

Achani amedokeza kuwa wakaazi wa maeneo yanayoathirika na tatizo la ukosefu wa maji  kwenye kaunti hiyo wataanza kupata bidhaa hiyo muhimu punde tu  hatua za mwisho za ujenzi wa bwawa hilo zitakapokamilika hivi karibuni.

Bwawa hilo aidha linatarajiwa kuwawezesha wakulima kwenye kaunti  hiyo kuimarisha  shughuli zao za  kilimo kwa  kuwawezesha kukuza mazao mashambani kupitia zoezi la unyunyiziaji maji.

Miongoni mwa miradi mikubwa ya maji inayoendelezwa hivi sasa  na ambayo ilizinduliwa mwaka jana na utawala wa mvurya  inajumuisha ile ya bwawa la  Mwache na Makamini iilioyogharimu shilingi bilioni 20 na bilioni 1.2 mtawalia.

https://glimtors.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287