Wakaazi Vanga waitaka serikali ya kwale kutambua vivutio vya utaliii eneo hilo

Baadhi ya wakaazi katika eneo la Vanga kaunti ya Kwale wameirai serikali ya kaunti hiyo chini ya uongozi wa  gavana mpya Fatuma Achani kutambua na kuhifadhi  vivutio vya utalii vinavyopatikana katika eneo hilo.

Wakiongozwa na Mohammed Feruz Wakaazi hao wanasema kuwa licha ya Kisiwa cha vanga kuwa na utajiri wa Historia wa  matukio makubwa yaliyowahi kutokea duniani,  bado serikali ya kaunti ya Kwale haijatambua vivutio  vya utalii katika eneo hilo.

Feruz amedokeza kuwa miongoni  mwa matukio hayo ni pamoja na vita vya pili vikuu vya dunia vilivyotukia   eneo hilo ambapo wareno ,wajerumani na waarabu waliacha majengo ya  kihistoria baada ya kukamilika kwa vita hivyo.

Wakati huo huo amesema kuwa inasikitisha kuona  kuwa vivutio vya utalii kama Fort Jesus pamoja na kile cha  Gede vimehifadhiwa  vizuri na serikali ilhali vivutio sawia na hivyo vinavypatikana kwenye kaunti ya kwale bado havijahifadhiwa.

kauli yake imeungwa mkono na Nuru Kombo ambaye ameishinikiza serikali ya kaunti ya Kwale  kutumia  vivutio hivyo  ili kutengeneza nafasi za ajira  kwa vijana sawia na kuimarisha  biashara katika sekta hiyo.

Itakumbukwa kuwa mapema mwaka huu Waziri wa utalii kwenye kaunti hiyo Nasib Nyahi aliagiza kuramanishwa upya na kutambuliwa kwa vivutio vyengine vya utalii  ili kupiga jeki sekta hiyo kikamilifu.

https://itweepinbelltor.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287