Kalonzo ajiondoa katika kinyang’anyiro cha uspika

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amejiondoa katika kinayang’anyiro cha kuwania  kiti wa uspika katika bunge la kitaifa na lile la seneti.

Hatua ya Kalonzo inajiri kufuatia  mkutano wa baraza kuu la chama cha Wiper hapo jana ambalo linasemekana  kumshawishi kalonzo kuachana na azma hiyo na badala yake ajikite katika kujenga jina lake kisiasa.

Hatahivyo wabunge wengi wanaamini kuwa Mrengo wa Azimio una  idadi ndogo ya wabunge amabo wangemwezesha Kalonzo kunyakua kiti hicho  kufuatia kujiengua kwa vyama tanzu vilivyojifungamanisha na mrengo huo kabla ya uchaguzi.

Hayo yanajiri huku miungano yote hiyo ya kisiasa ikitarajiwa kukutana na wabunge wao hii leo ili kujadiliana maswala kadhaa kabla ya vikao vya bunge la kumi na tatu kuanza rasmi hapo kesho.

Ikumbukwe kalonzo alikuwa tayari amwechukua fomu  za uteuzi wa kiti cha uspika katika bunge la kitaifa na llle la seneti.

https://ptauxofi.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287