wakaazi wa kongowea wataka mradi wa ujenzi wa vyoo makaburini kusitishwa

Shirika la utetezi wa Haki za kibinaadamu la Haki yetu Limetoa makataa ya siku Saba Kwa Serikali inayomaliza hatamu yake  ya kaunti ya Mombasa  kusitisha mradi wa  ujenzi wa vyoo katika makaburi ya Umma eneo la Kongowea la sivyo ichukuliwe hatua za kisheria.

Shirika Hilo  linadai kuwa kuwa mradi huo wa ujenzi wa vyoo  ambao unafadhiliwa na Banki kuu ya dunia ulitekelezwa pasi na kuwahusisha wakaazi wa eneo hilo  ambao wamewazika wapendwa katika makaburi hayo.

Hatahivyo akizungumza  na wanahabari katika eneo hilo afisa anayesimamia maswala ya ardhi katika shirika la Haki Yetu Munira Ali ameitaka tume ya kitaifa ya  ardhi  NLC kujitokeza wazi  na kutoa ripoti kamili kuhusiana na mradi huo,wakati huo huo  akiishinikiza serikali ya kaunti ya Mombasa kukomesha utupaji taka katika makaburi Eneo hilo.

 

 

Kauli yake imeungwa mkono na Julis Wanyama kutoka shirika hilo la Haki yetu ambaye ameitaka banki kuu ya dunia kusimamisha mara moja  ufadhili wa mradi huo huku  akimtaka gavana mteule wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir kujitokeza na kuchukua hatua muafaka sivyo wamchukulie hatua za kisheria.

Kwa upande wao wakaazi wa eneo la  hilo wameonyesha ghadhabu yao kuhusiana na ujenzi wa vyoo unaoendelezwa katika makaburi hayo  huku wakizitaka asasi husika kuingilia kati na kusitisha ujenz huo  sawia na Utupwaji wa taka katika makaburi.

https://yonhelioliskor.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287