Hajji asema hana ushahidi wa Naibu Rais william Ruto kuhusishwa na sakata la arror na kimwarer

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP Nurdhin Hajj ameweka wazi kuwa hakuna ushahidi wowote unaomuhusisha Naibu wa rais William Ruto kuhusiana na sakata ya mabwawa ya Arror na Kimwarer

Kulingana na Hajji japo Ruto anahusishwa na kesi hiyo ila jina lake halimo kwenye faili zilizoko mahakamani.

Hajji aidha amesisitiza kwamba hatakubali watu kupigana kisiasa katika kashfa za arror na Kimwarer kwenye afisi yake.

Wakati huo huo Hajji amesema kuwa afisi yake imepiga hatua katika masuala ya kukabili ufisadi ikiwemo ile kesi ya Waluke `huku akisisitiza kwamba kesi ya Arror na Kimwarer ambayo bado iko mahakamani ameipa kipau mbele zaidi kuitatua.

 

https://bouhoagy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287