Mahakama kuu Mombasa Imeiagiza Tume ya IEBC kumuidhinisha Sonko Kuwania ugavana Mombasa
Mahakama kuu mjini Mombasa imeiamuru Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kumuidhinisha aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sinko kuwania ugavana kaunti ya Mombasa.
Katika uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo chini ya jopo la majaji watatu, wamesema kuwa Tume ya IEBC ilienda kinyume na sheria kumzuia sonko kuwania ugavana kaunti hiyo licha ya kuwa na stakabadhi husika.
Jopo hilo la majaji watatu lililo ongozwa na Olga Sewe,Stephen Githinji na Ann Ong’injo ,limesema IEBC haikustahili kumzuia sonko kugombania kiti hicho huku IEBC ikiagizwa kumjumuisha sonko na mgombea mwenza wake Ali Mbogo kwenye karatasi za kupigia kura kaunti ya Mombasa.
Ikumbukwe sonko analenga kumrithi gavana wa sasa Ali Hassan Joho kwa tiketi ya chama cha Wiper.