MUHURI YAITAKA SEREKALI YA MOMBASA KULIPA SHILINGI MILIONI 126 KWA KAMPUNI MOJA YA MAWAKILI ILIYO KUWA IKIWAKILISHA KAUNTI KWENYE KESI ZOTE

Shirika la kutetea haki za binadamu la MUHURI limeitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kulipa madeni yote kabla ya serikali hio kuondoka mamlakani.

Mwenyekiti wa shirika hilo Khelef Khalifa amesema kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa inadaiwa zaidi ya shilingi milioni 126 na kampuni moja ya mawakili ambayo imekuwa ikiwakilisha kaunti kwenye kesi zote kuanzia mwaka 2008 hadi 2020.

Wakati uo huo Khalifa amemtaka gavana anayeondoka Hassan Ali Joho kuwachukulia hatua wafanyikazi wake wanaokabiliwa na shutuma za ufisadi wakati huu ambao kaunti hiyo inatarajia gavana mpya baada ya uchaguzi mkuu ujao.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287