Afueni Kwa Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Seikali ikiahidi kuangazia maslahi yao Zaidi

kwa muda mrefu jamii ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi nchini imekuwa ikibaguliwa kwa kutojumuishwa  katika nyadhfa  mbali mbali  huku wengi wao  wakiaga dunia kutokana na saratani ya ngozi kwa ukosefu wa  matibabu bora.

Madhila hayo huenda yakazikwa katika kaburi la sahau endapo Serikali ya kitaifa itaweka mikakati na mipangilio muafaka ya Kuwawezesha walemavu wa Ngozi nchini kujikimu kimaisha.

Akizungumza wakati wa mashindano ya urembo ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaliyoandaliwa katika kaunti ya Mombasa Seneta Maalum Isaack Mwaura amewataka wakenya kuwaenzi watu wa jamii hiyo akiwataja kama  wenye uwezo  Mkubwa wa kufanya kazi zikiwemo katika jeshi na pia kushiriki katika michezo mbalimbali.

Kwa upande wake  mkurugenzi mkuu wa baraza la walemavu  hapa nchini kenya Harun hassan amesema Serikali imekuwa ikiwasaidia  watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kuwatengea  miradi mbali mbali ili kuwawezesha kujikimu kimaisha  sawia na kuwapa mafuta maalumu ya kujipaka ili wajikinge na Jua .

Vile vile  mkurugenzi huyo amebainisha kuwa seriakali hutoa ya  matibabu ya bure kwa watu wa jamii hiyo  waliyopatwa na saratani ya ngozi na pia kuwapatia furasa ya kupata elimu na kujiendeleza kimasomo

https://glimtors.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287