Abdulswammad Amteua Francis Thoya Kama Mgombea Mwenza kuwania Kiti cha Ugavana Mombasa
Mwaniaji wa kiti cha ugavana kaunti ya mombasa kupitia chama cha ODM Abdulswamad Sharif Nassir amteua Francis Thoya kama mgombea mwenza wake katika safari yake ya kusaka kiti cha ugavana.
Akiongea katika hafla ya kumuidhinisha mgombea mwenza wake Abdulswamad ameendelea kujipigia debe na kuweka wazi sera zake kwa wakaazi wa kaunti ya mombasa huku akiahidi kuzitimiza iwapo atachaguliwa kama gavana katika uchaguzi wa Agosti 9.
Kwa upande wake Fransic Thoya ambae ndie ametuliwa kama naibu gavana amewataka waakazi wa kaunti ya mombasa kuwakataa viongozi watakaowagawanya kwa misingi ya kidini na kikabila .
Aidha thoya amempongeza Abdulswammad nakuahidi kushirikiana nae ili kuhakikisha anainyakua nafasi hiyo ya ugavana.