Hisia Za Wana Mombasa Baada ya PAA Kujiunga na Kenya Kwanza

Uamuzi wa chama cha PAA kuhamia kwenye muungano wa Kenya kwanza sasa umeibua hisia mesto kwa wakaazi wa Mombasa huku baadhi wakionyesha kugadhabishwa na uamuzi huo na wengine kukubaliana  na uamuzi huo.

kulingana na baadhi ya watu, Amason Kingi alistahili kusikiliza maamuzi ya wafuasi wake kuhusu chama cha PAA kujiunga na Kenya kwanza kuliko kuchukua maamuzi ya haraka na kusisitiza kwamba kingi alichukua uamuzi huo kwa lengo la kujifaidi kibinafsi.

Kwa upande mwengine baadhi wamesema kwamba kingi alichukua maamuzi ya busara kujiunga na kenya kwanza wakisema kuwa ni haki ya kikatiba ya kila mkenya kuchagua chama ama muungano wenye manufaa.

https://eechicha.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287