Wafanya biashara wakuuza vinyago kaunti ya kwale walalamikia kuvunjwa kwa vibanda vyao

Wafanyibiashara katika eneo la Diani kaunti ya Kwale wanalalamikia hatua ya serikali ya kaunti hiyo kubomoa vibanda vyao vya biashara bila ya kupewa ilani ya kuondoka na serikali ya kaunti hiyo.

Wafanyibiashara hao wanaouza vinyago na bidhaa zingine kwa watalii wamepinga vikali hatua hiyo inayolenga kutoa nafasi kwa mradi wa ujenzi wa mabomba ya kupitisha maji katika eneo hilo.

Hata hivyo wafanyibiashara hao wamemtaka gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya kuingilia kati ili kuona kwamba zoezi hilo linasitishwa sawia na kuwalipwa fidia ya hasara ya mali yao huku mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji maji Kwale (KWAWASCO) Eric Parmet akiahidi kuwa wafanyibiashara walioathirika watafidiwa.

 

 

https://omoonsih.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287