MAKALA: KOVU LA UGAIDI

Maafisa wa polisi wa kituo cha Central mjini Mombasa wakikimbilia usalama wao baada ya uvamizi wa magaidi 2016. Picha Maktaba/Kwa Hisani

Katika malezi mama na baba wana jukumu kubwa katika maangalizi ya watoto. Hata hivyo kaida ya muda mrefu na mara nyingi mtoto anapoharibika basi moja kwa moja kidole cha lawama huelekezwa kwa mama.

Suala la vijana kupotea kutokana na kushawishiwa kuchukua misimamo mikali, au kutumiwa vibaya na hata kujiunga na makundi ya kigaidi kama vile Al-Shabab limekuwa tatizo ambalo limepelekea majonzi tele katika jamii. Na hasa mama akionekana kuahtirika pakubwa.

Makala haya ya KOVU LA UGAIDI yaliyoandaliwa na Ramadhan (Mjomba) Rashid na kutiwa sauti naye Solomon Zully yameshughulikia athari ya vijana wanaojihusisha na ugaidi, vilio na malalamishi ya baadhi ya akina mama waliochiwa makovu ya kudumu kutokana na suala hilo.

 

Maafisa wa polisi wa kituo cha Central mjini Mombasa wakikimbilia usalama wao baada ya uvamizi wa magaidi 2016. Picha Maktaba/Kwa Hisani

Tulizungumza na akina mama mbalimbali kuona ni vipi vijana wanaweza kujinasua katika janga hili kupitia uangalizi wao.

Mwishowe tunaangazia umuhimu wa idara mbalimbali ikiwemo ya polisi na vijana kuja pamoja kuimarisha uhusiano mwema, huku viongozi serikalini wakitakiwa kuwawezesha vijana kwa kuwaekea miradi ya kudumu ya kujiendeleza kimaisha. Jamii nayo ikihimizwa kuwajibikia suala la malezi vilivyo.

Bonyeza kusikiliza:

https://tobaltoyon.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287