MAKALA: Chimbuko la Magenge Mombasa

Bango katika mojawapo ya maskani na kundi la Wakali Kwanza. Picha kwa Hisani

Makala: Chimbuko la Magenge Mombasa, NA MJOMBA RASHID/GEOFFREY CHIRO

Kaunti ya Mombasa, mji mkongwe Afrika Mashariki ni kaunti iliyo kivutio cha watalii kukotokana na bahari na mandhari ya kupendeza.
Lakini kwa siku za hivi karibuni taswira imekuwa ikibadilika na uzuri wake kutiliwa shaka.

Hili ni kutokana na kuchipuza kwa magenge magenge kadha wa kadha ya kihalifu yanayowahangaisha wakaazi viungani mwa mji wa Mombasa hasa maeneo ya Kisauni, Likoni, Nyali na Mji wa Kale.

Makundi kama vile Wakali Kwanza, Wakali Wao, Wajukuu wa Bibi, Chafu miongoni mwa makundi mengine hayajakuwa kikwazo tu kwa usalama bali pia tishio kwa maendeleo na kuimarika kiuchumi kwa kaunti hii.

Bango katika mojawapo ya maskani na kundi la Wakali Kwanza. Picha kwa Hisani

Tukio la hivi punde zaidi ni shambulizi lililodaiwa kutekelezwa na kundi lililochipuka hivi karibuni la 86 Batalion katika eneo la Frere Town eneo bunge la Nyali.

Maafisa wa polisi wakiwakamata baadhi ya washukiwa wa uhalifu wa magenge Mombasa. Picha kwa Hisani

Katika Makala haya tulizungumza na waathiriwa wa magenge hayo, vijana waliojiunga au kuunda magenge na kuvalia njuga athari yake na njia mwafaka za kukabiliana na uozo huo.

Bonyeza Kusikiliza Makala hayo yaliyoandaliwa na Ramadhan Rashid na kutiwa sauti na Geoffrey Chiro.

https://itweepinbelltor.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287