Nitaimarisha maisha ya wakaazi wa Majengo Mwembe Tayari nikichaguliwa 2022-Asema Nabeel Khamis Salim.

Muwaniaji wa kiti cha uwakilishi wadi cha Majengo Mwembe tayari Nabeel Khamis Salim ameahidi kuimarisha maisha ya wakaazi wa wadi hiyo iwapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuuwa mwaka 2022.

Nabeel ambaye anagombania wadhfa huo kupitia chama cha UDA amesema atatafuta suluhu za kudumu kwa shida ambazo wakaazi hao wanapitia ikiwemo ukosefu wa kazi ,kudorora kwa huduma za afya miongonimwa huduma zengine muhimu za kiserikali.

 

Aidha Nabeel amewataka wanasiasa kuacha kutumia vijana ili kutimiza malengo yao kisha kuwaacha bila kuwapatia fursa za kujiendeleza kimaisha.

Akidai kuna haja ya viongozi kuwajengea misingi ambayo itawapatia maisha bora hata baada ya kipindi cha siasa.

 

 

Vilevile Nabeel amewarai vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kama wapiga kura ili kuchagua viongozi ambao wataskiza vilio vyao na kuwakomboa katika maisha ya dhiki ambayo wanapitia.

 

 

https://ptauxofi.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287