Hakuna muwaniaji anayependelewa katika ODM- Asema Mwenyekiti Mohamed Hamid-DEE.

Chama cha ODM kaunti ya Mombasa kimewahakikishia uteuzi wa huru na haki wagombeaji mbalimbali wa nyadhfa za uwakilishi wadi katika kaunti hiyo kupitia chama hicho.

Akizungumza na wanahabari katika mkutano uliyowakutanisha wawaniaji wa viti hivyo kupitia chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu, mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa Mohamed Khamid Khamis almaarufu Dee amesema kuwa hakuna kiongozi anyependelewa na chama hicho na kwamba chini ya hatamu yake kama mwenyekiti atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha kuwa uteuzi wa chama hicho unafanyika kwa njia ya huru na haki.

Dee Aidha amewataka wawaniaji hao kuwahimiza wananchi wa kaunti ya Mombasa kujitokeza kwa wingi na kujisajili kama wapiga akisema kuwa idadi ya watu waliyojiandikisha kufikia sasa katika kaunti hiyo ni ndogo mno.

Wakati huo huo amewahimiza wagombeaji hao kumpigia debe kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga kama Rais wa tano wa taifa hili pamoja na kuwahasa wananchi kujisajili kwa wingi katika chama hicho.

 

Kwa upande wake katibu wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa Geofrey Busaka ametoa wito kwa wawaniaji hao kuendesha siasa kwa njia ya amani na kuwarai kusalia chamani hata baada ya kura za mchujo.

Aidha katika mkutano huo chama hicho kiliwapokea wagombeaji tisa waliyojiunga nacho kutokea vyama vyengine.

https://itweepinbelltor.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287