Vijana wakike wamehimizwa kujihusisha katika maswala ya uongozi.

Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Mombasa wamewataka vijana wa kike kujihusisha katika maswala ya uongozi wa vyama na ule wa kitaifa ili kutumikia jamii.

Wakiongozwa na mgombea wa kiti cha uwakilishi wa kike kaunti ya Mombasa ZamZam Mohammed amesema kuna haja ya wasichana kupewa nyadhfa za uongozi sawia wenzao wa kiume kwani ni haki yao ya kikatiba.

Zamzam akiwataka wafuasi wa ODM kumuunga mkono Zubeda Mikwara ili kuweza kuchaguliwa kama kiongozi wa vijana katika chama cha ODM kaunti ya Mombasa kwani ni msichana ambaye amepigania kukiimarisha chama na kuhakikisha kina nawiri katika kaunti ya Mombasa pamoja na kuwaleta vijana pamoja.

Kwa upande wake mbunge wa Jomvu badi Twalib amesema mtu yeyote ambaye amekuwa akikitumikia chama na kuwashughulikia wananchi ipasavyo basi ana haki ya kupewa nyadhfa ya uongozi. Badi akiunga mkono hatua ya vijana wasichana kupewa nyadhfa za uongozi katika chama cha ODM.

Kwa upande wake katibu wa vijana katika chama cha ODM Zubeda Mikwara  amesema iwapo atachaguliwa kuwa kiongozi wa vijana katika chama cha ODM atahakikisha vijana wa kisichana wamewezeshwa zaidi na kupewa nyadhfa mbalimbali za uongozi.

Aidha amewata wafuasi wa ODM kujiandikisha kuwa wanachama wa kudumu.

 

 

https://tobaltoyon.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287