Taufiq Balala awahimiza viongozi kuwekeza katika michezo ili kuimarisha vipaji katika kaunti ya Mombasa.

Waziri wa miundo msingi katika kaunti ya Mombasa Taufiq Balala amewataka viongozi kujihusisha kikamilifu katika maswala ya michezo.
Akiongea katika kaunti ya Mombasa Balala amesema kuna haja ya viongozi kudhamini timu za mpira wa miguu ili kuhakikisha talanta zinatambulika na kuendelezwa katika kaunti ya Mombasa.

Balala amesema ni gharama sana kuendesha shughuli ya timu jambo ambalo linafanya kutoendelea kwa mpira wa miguu katika kaunti ya Mombasa.

Aidha Taufiq amesema kuna haja ya kubadilisha uongozi katika sekta ya michezo ili kufufua sekta ya hiyo na kutoa nafasi kwa vijana kujiendeleza kupitia michezo.

Vilevile Taufiq amewaomba viongozi wa timu kukumbatia mbinu muafaka ili kuvutia wawekezaji watakao dhamini na kuendesha shughuli zao ikiwemo kuvutia mashabiki zaidi katika Timu.