Ndondi yapigwa jeki katika wadi ya Mjambere na Mama Nuru Saadat.

Mashindano ya ndondi ya Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi wa mjambere Mama Nuru Saadat yaliyofanyika katika uwanja wa Kadongo yakamilika. Mashindano hayo ya siku moja yaliyo wavutia wanandondi Zaidi ya ishirini kutoka sehemu mbalimbali ya wadi ya mjambere na maeneo mengine ya kaunti ya Mombasa yalikuwa ya aina yake kuwahi kutokea katika kaunti ya Mombasa. Mapigano kumi yalishuhudiwa huku wanandondi wakionyesha ustadi wao wakurusha masumbwi.

Alex Masika mwenye umri wa miaka 26 alipatiwa tuzo ya mwanandondi bora katika mashindano hayo akizawadiwa kikombe pamoja na cheti,wengine waliotuzwa ni pamoja na Lyncolyn Onyango 11,Haji Ramadhan,Silas Nyanje,Abdallah Juma,Said Pandu,Marc Gregory,Tony Juma,Hamza Said na Abdallah Athumani.

Mdhamini wa mashindano hayo Mama Nuru Saadat amesema ataendelea kukuza vipaji vya vijana na kuviendeleza ili kuhakikisha wamejiendeleza kimaisha na wametambulika na jamii.

Kwa upande wake muandaaji wa mashindano hayo Juma  Mashuhuri amesema haikuwa rahisi kuandaa mashindano hayo kutokana na changamoto za kupata ulingo ikizingatiwa ni ring mbili tu zilizopo katika kaunti ya Mombasa.

Mashururi akipongeza hatua ya mama Saadat kukuza vipaji kwani vipaji ni ajira inayolipa sana.