ODM kuandaa mkutano na wagombeaji mbalimbali wa viti vya uwakilishi wadi Mombasa.

Chama cha ODM katika kaunti ya Mombasa kuandaa mkutano na wagombeaji mbalimbali wa viti vya uwakilishi wadi katika kaunti hiyo kupitia kwa chama hicho ili kuhakikisha wagombeaji hao wanaendesha siasa zao kulingana na sheria na kanuni za chama hicho,sawia na kujiandikisha kuwa wanachama wa kudumu.


Akizungumza na wanahabari katika afisi kuu ya chama hicho katibu mkuu wa chama hicho kaunti ya Mombasa Geofrey Busaka amesema chama hicho kimenuwia kuaanda mkutano huo ili kuhakikisha wagombeaji hao wanaendeleza kampeni zao kulingana na sheria na kanuni za chama hicho.


Aidha wagombea hao wametakiwa kujiandikisha kuwa wanachama wa kudumu kabla ya kuhudhuria mkutano huo ili kutumikia chama hicho inavyosahili.

 

Busaka aidha amesema mkutano huo utapeana fursa kwa wagombeaji hao na usimamizi wa chama hicho kuweka mikakati mwafaka ya kuandaa kura za amani na huru katika mchujo wa chama hicho katika kaunti hiyo.

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama ODM kaunti ya Mombasa ,Mohammed Hamid Khamis amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kujitokeza na kujisajili kama wapiga kura katika kaunti hiyo ili kuweza kuchagua viongozi waadilifu na walio na malengo yakuwendeleza kaunti hiyo .


Vilevile Mohamed amewataka wafuasi wa chama cha ODM kujiandikisha kuwa wanachama wa kudumu ili kuwawezesha wao kushiriki kura za mchujo.