TOENI SHAKA, ODM NI YA KILA MTU,ASEMA MWENYEKITI DEE.

Huku vuta ni kuvute likienda kupamba moto Kuhusu matamshi ya naibu Kinara wa Chama Cha ODM, Hassan Joho ya kuonekana kuunga Mkono mgombea, Abdulswamad Sharrif Nassir, Mwenyekiti wa Chama hicho katika Kaunti ya Mombasa, Mohammed Khamis maarufu Dee amejitokeza na kupinga madai kuwa Chama kinapendelea wagombea Fulani.

Dee amesema kuwa Chama Cha ODM ni Cha kila mtu na kusisitiza kuwa mchujo wa Chama utakua wa huru na haki.

Kuhusu Matamshi ya Joho, Dee amesema kuwa hakuona kuwa alipendeza mgombea flani na huenda vyombo vya Habari vilimnukuu vibaya.

Dee amesema kuwa Kinara wa ODM,Raila Odinga aliweka wazi kuwa uamuzi wa atakaye peperusha bendera ya ODM utaamuliwa na Wananchi wenyewe katika kura za mchujo ambazo zitaendeshwa na bodi ya kitaifa ya Chama