JOHO ANAVURUGA ODM, ASEMA IDRIS.

Matamshi ya naibu Kinara wa Chama Cha ODM, ambaye pia ni Gavana wa Kaunti ya Mombasa, Hassan Joho ya kuonekana kumuunga Mkono mgombea wa Kiti Cha Ugavana kupitia ODM, Abdulswamad Sharrif Nassir yameonekana kuleta mtafaruku ndani ya Chama hicho.

Mkuu wa kampeni za Suleiman Shahbal, Major Idris Abdulrahman amesema kuwa Joho Anaenda kinyume na matakwa ya Chama kwa kuunga upande mmoja wa wagombea wawili wakuu wa tikiti ya Chama Cha ODM katika kinyanganyiro Cha Ugavana mwaka wa 2022.

Idriss amesema kuwa Kinara wa ODM, Raila Odinga aliweka bayana kuwa uamuzi wa atayepeperusha bendera ya ODM kati ya Suleiman Shahbal na Abdulswamad Shariff Nassir utasalia kwa Wananchi wenyewe.

Idris amesema kuwa Joho anarudia makosa aliyoyafanya katika Uchaguzi mdogo wa Msambweni ambapo mgombea aliyekuwa akimuunga mkono,Omar Boga aliangushwa.

Kwa upande wake,Mgombea Suleiman Shahbal ambaye alihama kutoka Jubilee na kujiunga na ODM, amesema kuwa hatabanduka katika Chama hicho Hadi pale wapiga kura watakapo toa uamuzi katika kura za mchujo wa Chama mwakani