DENMAK FC mabingwa wa makala ya pili ya Rashid Abdallah Super Cup.

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Makala ya pili ya kipute cha Rashid Abdallah Super Cup yalifikia ukingoni wikendi hii , huku vijana wa Denmak FC wakitwaa ubingwa wa makala ya mwaka huu walipowanyamazisha mahasimu wao Lazium FC katika fainali ya kukata na shoka iliyogaragazwa kwenye Uga wa shule ya msingi ya Waa ,iliyoko gatuzi dogo la Matuga kaunti ya Kwale.

Licha ya Lazium FC kuonekena kurudi kwenye mchezo walipo sawazisha mnamo dakika za lala salama kutokana na vijana wa denmak kutangulia mnamo kipindi cha kwanza, bado walishindwa kuutwaa ubingwa baada ya mechi hiyo kuelekea kwa mikwaju ya penalty ilipoishia sare ya moja bin moja katika muda wa dakika 90.

Vijana wa denmak walionyesha weledi wao kwenye mikwaju ya penalty walipopachika mikwaju yote mitano huku Lazium FC wakipoteza mkwaju mmoja uliogonga mwamba  na kuyazima matumaini yao.

Denmak walitia kibindoni shilingi laki moja pesa taslimu, kombe ,jazi set moja ,mipira ya soka miwili pamoja na viatu vya kuchezea.

Licha ya kupoteza fainali hiyo Lazium FC walijitilia kibindoni shilingi elfu thelathini na mpira mmoja wa soka.

Kwa upande wa kina dada Swabrina walionyesha mchezo mzuri walipowalaza kina dada wa Kombani queens goli moja bila jawabu na kuhakikisha wanipeperusha bendera ya kina dada, huku vijana wa nyumbani wa Marika youth wakiwalaza vijana wa Rising Stars goli mbili kwa sufuri na kutawazwa mabingwa katika kitengo cha vijana chini ya umri wa miaka kumi na mitano.

Katika kitengo cha wazee  ,Ng’ombeni All Stars waliwaza Shikaadabu Veterans goli moja bila jawabu na kuhakikisha wanatia mfukuno shilingi elfu hamsini ,kombe pamoja na mipira miwili ya soka.

Rashid Abdallah kwa upande wake ameonekana kuwamiminia sifa vijana walioshiriki kipute hicho kutokana na hali ya juu ya nidhamu waliyoandikisha akisema ni dhahiri lengo lake kuu amelitimiza.

 

Wageni walioalikwa kushudia karambe hizo walimsifia sana Rashid kutokana na kuandaa kipite hicho wakisema  hiyo ndo nia pekee kuhakikisha vipaji vya vijana vinapewa kipaumbe kauli iliyoonekana kuungwa mkono na mkufunzi wa klabu ya Bandari Cassa Mbungo

Hata hivyo aliyekuwa nahodha wa zamani  wa timu ya taifa Harambee Stars Macdonald Mariga ametoa wito kwa wasimamizi wapya wa shirikisho la soka kukuza vipaji mashinani kwani vipaji vipo nchini na vimekuwa vikiachwa pasi na kushughlikiwa.