Chama cha ODM kiko imara kaunti ya Mombasa,Mwenyekiti Mohamed Hamid-Dee amuhakikishia Raila Odinga.

Mwenyekiti wa Chama cha ODM kaunti ya Mombasa Mohamed Hamid Khamis amemuhakikishia kinara wa chama hicho Raila Odinga kuwa chama cha ODM kiko imara na maarufu katika kaunti ya Mombasa.

Akizungumza kwenye mkutano na wazee uliowaleta pamoja wakaazi na viongozi mbali mbali kutoka kaunti ya Mombasa katika ukumbi wa shule ya msingi ya Sheikh Zeyyed huko Nyali Mohamed amemtaka Raila Odinga kutoa shaka kwani  juhudi zake za kuimarisha chama hicho ziko wazi na zinaonekana.

 

Mohamed pia amemuhakikishia Raila Odinga  ushindi kwani dalili zote ziko wazi za yeye kuwa Rais wa tano wa Taifa la Kenya ifikapo mwaka 2022.

Mohmmed amekuwa akipokea pongezi kutoka kwa viongozi pamoja na wafuasi wa chama hicho kwa jinsi anavyokiendesha vyema chama hicho tangu alipochukuan hatamu.