ADEL BALALA ATWAA TUZO YA GOFU YA KENYA OPEN 2021.

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Baada ya msururu wa mwaka huu wa michuano ya Gofu ya Kenya Open nchini ,Adel Balala wa Nyali Golf Club  aliibuka mshindi wa msururu huo kitengo cha amature akiwapiku wapinzani wake wa karibu Michael Karanga wa Kiambu Golf Club pamoja na John Lerjma wa Kenya Railways.

Akiongea baada ya kutajwa mshindi wa msururu huo Adel amewashukuru wadhamini wake Kenya vision 2030 kwa kujitolea kusimama naye kwenye mchezo huo.

Tayari Adel amesafiri kuelekea  huko Milki za kiarabu kwa michuano ya kifahari ya Abu Dhabi Golf  Amature Championship,akisema anaimani ataendelea msururu wa matokeo mazuri kwani ari yake kubwa ni kuhakikisha anazidi kuandikisha historia  kwenye mchezo huo.

Aidha kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa taasisi ya Kenya Vision 2030 Kenneth Mwige amesema ni fahari kuona nambari tatu za kwanza zinanyakuliwa na vijana waliowadhamini akisema kama taasisi wako imara kuhakikisha wanawashika mkono wanamichezo wa tabaka mbali mbali humu nchini kuhakikisha tu wanainua viwango vya michezo.

Mwige vile vile amezitaka taasisi zaidi kujitokeza kama wadhamini  wakati wa michuano ya magical Kenya open itakayo andaliwa hapo machi mwaka 2022,ili kuhakikisha kuwa wanaukuza mchezo wa golf nchini.