Mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa Mohamed Hamid-DEE awatahadharisha wagombea dhidi ya matamshi ya chuki
Mwenyekiti wa chama cha ODM katika kaunti ya Mombasa Mohammed Hamid amewatahadharisha wagombea katika chama cha Odm dhidi ya kujipiga kifua na kutumia kauli ambazo huenda zikawagawanya na kusababisha chuki miongoni mwa jamii.
Akiongea katika makao makuu ya chama hicho mtaa wa Ganjoni kaunti ya Mombasa baada ya kumkaribisha mgombea wa kiti cha ubunge cha Mvita Mohammed Machele,mwenyekiti huyo amesema iwapo kuna kiongozi ambaye hatafurahishwa na jinsi mambo yanavyoendeshwa katika chama hicho basi anatakiwa kufata utaratibu uliowekwa na chama ili kupata haki.
Aidha Muhammed amechukua fursa hiyo kuwarai wafuasi wa chama cha ODM kujisajili kuwa wanachama ,akiweka wazi kuwa wanachama pekee ndio wataoshiriki katika kura za mchujo hivyo kuwataka kufanya uamuzi wa kujiandikisha mapema ili kumuwezesha mgombea wao kuchukua tiketi iwapo atashinda katika mchujo.
Vilevile Muhamed amezidi kuwahakikishia wafuasi wa chama chama cha ODM kuwa mchujo wa chama hicho utakuwa huru na haki. Akiwataka wafuasi kuzidi kuwa na imani na uongozi wake.