RASHID ABDALLAH SUPER CUP NGUZO KATIKA KUMALIZA UHASAMA KWALE.
Jamii imetakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaubadilisha mtazamo wa maisha miongoni mwa vijana humu nchini kwani uhasama unaonekana kuongezeka kila uchao
Akiongea wakati wa uzinduzi wa makala ya pili ya michuano ya Rashid Abdallah Super Cup,katika uwanja wa shule ya msingi ya Waa eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale, Rashid amesema michezo huenda ikawa nguzo muhimu katika kufanikisha hilo.
Michuano hiyo iliyoanzishwa ili kutoa hamasisho kwa jamii dhidi ya kushabikia uhalifu pamoja na kumaliza uhasama miongoni mwa vijana , inahusisha timu za kandanda kwa wazee,wakina mama , vijana pamoja na timu za watoto.
Katika michuano iliyogaragazwa wikendi hii ,timu ya vijana ya Wailers ilitoka sare ya goli mbili (2:2) dhidi ya Albion ,upande wa kina dada Swabrina ikawaadhibu Kombani starlets goli tatu bila jawabu (3:0) na upand wa wazee likoni legends ikawalazimisha WAA legends sare vilevile.
Aidha michuano hiyo inatarajiwa kuingia katika hatua ya robo fainali wiki hii huku mabingwa wa michuano hiyo wakitarajiwa kujizolea zawadi kem kem kutoka kwa wadhamini.