Wazee wa eneo bunge la Mvita wamuidhinisha Machele kuwa mgombea wao.

Mgombea wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Mvita Mohamed Soud Machele ameidhinishwa rasmi na wazee pamoja na viongozi wengine katika eneo bunge hilo kama mgombea wao wa ubunge.

 

Katika mkutano uliowaleta pamoja wazee na viongozi wa eneo la Mvita uliofanyika katika ukumbi wa Paris,Machele ametawazwa rasmi kama chaguo la wakaazi wa Mvita katika kinyanganyiro hicho cha ubunge huku wakiahidi kusimama nae kuhakikisha anatimiza azma yake.

 

Akiwahutubia wakaazi katika mkutano huo,Machele amesema kuwa ataangazia swala la elimu na kuimarisha uchumi wa eneo bunge la Mvita atakapochaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Machele akisema yeye ndio chaguo sahihi kwa wakaazi wa Mvita kwani anaelewa shida wanazopitia.

Kwa upande wake aliyekuwa meya wa mji wa Mombasa Ahmed Mohdhar, amewarai wananchi kumuunga mkono Machele huku akikitaka chama cha ODM kufanya kura za mchujo za haki.

Muhdhar akiahidi kusimama na Machele hata asiposimama na chama cha ODM

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287