Shahbal aahidi ufadhili wa masomo ya chuo kwa wanafunzi bora iwapo atachaguliwa kuwa Gavana 2022

Mfanyabiashara Suleiman Shahbal anayewania kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa ameahidi kufadhili wanafunzi wote kutoka Mombasa ambao watapata nafasi za kujiunga na chuo. Hii ni iwapo mfanyabiashara huyo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa gavana wa pili wa kaunti ya Mombasa katika uchaguzi ujao wa 2022.

Akizungumza katika eneo la Bombolulu alipokutana na wazee kutoka eneo bunge la kisauni,Shahbal amesema vijana wengi wamekuwa wakijiunga na magenge ya uhalifu na kujiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya kwa sababu ya ukosefu wa elimu na kazi.

Aidha shahbal amesistiza kuwa usaidizi wa karo haufai kutolewa kwa misingi ya kikabila au kujuana kwani kila mtoto ana haki ya kikatiba ya kupata elimu.

Wakati huohuo Shahbal ameazimia kuchukua wanafunzi 20 katika kila eneo bunge la Mombasa kwenda kusoma ngambo.

https://moonoafy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287