Makala: Athari ya Covid-19 kwa Shule za Mitaa ya mabanda, APBET Kaunti ya Mombasa

Shule za Mitaa ya Mabanda maarufu kama APBET Ni shule zinazotoa huduma ya masomo kwa ada ya malipo nafuu, maeneo ya mitaa ya mabanda hasa katika Miji Mikuu nchini Kenya na hutegemea malipo haba ya kila wiki au kila mwezi ya wazazi.
Kulingana na ripoti ya utafiti wa Shirika la DIGNITAS ya April 22, 2020, kabla ya ujio wa Korona taifa la Kenya lilikuwa na zaidi ya shule 5,000 za APBET, Kaunti ya Nairobi pekee ilikuwa na zaidi ya shule 3500, Mombasa ikiwa na shule 600 chini ya mfumo huo.
Shirika la DIGNITAS lilratibu kuwa familia 6 kati ya 10 Kaunti ya Nairobi ilikuwa ikiwasomesha watoto wao katika shule hizi, huku familia 3 pekee kati ya 10 zikiwa na uwezo wa kufikia shule za umma.
Ripoti ya utafiti wa Shrika la Financial Sector Deepening Kenya, FSD Kenya iliratibu kuwa asilimia 95% ya shule za APBET hugharamikia na kusimamia shughuli zao zote kutoka na ada ya karo wanayokusanya.

Je, Ujio wa Ugonjwa wa Virusi vya Korona,Covid-19 nchini mnamo Mwezi Machi 2020 kuliashiria nini katika mustakbali wa maendeleo na masomo kwa shule hizi?
Je, baada ya kufunguliwa shule tena zaidi ya miezi 6 baadaye, Je, shule za APBET zilirejelea masomo na kuendelea kuhudumu?
Ramadhan Rashid (Mjomba Rashid) ametuandalia Makala Sehemu ya 1 na ya 2 kubainisha uhalisia wa mambo na hatma ya shule hizo za APBET kaunti ya Mombasa.
Sehemu ya 1 ya makala:
Bonyeza usikilize
Sehemu ya 2: Makala ya ‘Athari ya Covid-19 kwa Shule za APBET’
Baada ya tangazo la Waziri wa Elimu nchini Prof. George Magoha kuruhusu ufunguzi wa shule awamu ya pili kwa madarasa yote mwezi Januari 2021 kwa kuzingatia masharti na kanuni za kudhibiti msambao wa Covid-19, Je, ni shule zote ziolifunguliwa?

Licha ya misukosuko hiyo, Inasemwa kuwa Penye mawimbi na milango ipapo na hakuna refu lisilokuwa na mwisho.
Sehemu ya 2: Bonyeza usikilize
Makala; Athari ya Covid-19 kwa Shule za APBET Kaunti ya Mombasa.