KFS Yavuta Jamii Kuzindua Mpango wa Kuhifadhi Mikoko Gasi

Serikali kupitia Idara ya misitu nchini (KFS) imezindua rasmi mpango wa kuishirikisha jamii katika zoezi la uhifadhi wa mikoko eneo la Gasi kaunti ya Kwale.

Mkurugenzi wa Idara hiyo Julius Kamau amesema kwamba mpango huo unalenga kupiga jeki juhudi za serikali za kulinda misitu ya mikoko katika eneo hilo.

Akizungumza katika msitu wa Gogoni, Kamau amesema kuwa mpango huo utatekelezwa katika jamii kwa muda wa miaka mitano.

Kwa upandewake mratibu wa vanga blue forest mwanarusi muafrika amesema wanajihusishwa na uhifadhi wa mikoko ili kulinda uhalisia wa mazingira.

Muafrika amesema kwa kupitia uhifadhi huyo wamepata milioni mia 3 na kuzindua miradi mbali mbali ya kusaidia jamii.

Kauli hiyo imetiliwa pondo na rahma rashidi ambae ni mratibu wa mikoko pamoja eneo la gazi amesema jamii ilitengwa na sasa suluhisho litapatikana