WENYEJI WA MADOGO, TANA RIVER WAITAKA KAMPUNI YA TAWASCO KUREJESHA USAMBAZAJI WA MAJI NDANI YA SIKU 21

PHOTO COURTESY

Uhaba wa maji huwenda ukasali kuwa tatizo Tana River na viunga vyake huku wakaazi wakiitaka kampuni ya TAWASCO kuwajibikia tatizo hilo kikamilifu

Wenyeji  wa mji wa Madogo kaunti ya tana River wameitaka kampuni ya maji na maji taka (TAWASCO)  kurejesha usambazaji wa maji katika mji huo chini ya siku 21.

Hayo yanajiri katika mkutano ulioitishwa kujadili tatizo la maji katika mji huo . Wakaazi wanadai kuwa  mabwenyenye  wanapata maji na kuendesha shughuli zao ilhali wengine wasiojiweza wasalia kulalama kuhusu uhaba  maji kwa takriban miezi sita sasa.

Hata hivyo wenyeji hao hawaoni sababu za kukosa maji kwani kuna vyanzo vya maji ikiwemo mito katika katika maeneo mbali mbali mji huo.