Bunge la Kaunti ya Mombasa laidhinisha uteuzi wa Omar Ali Shariff kuwa mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji wa umma na uhasibu

Bunge la Kaunti ya Mombasa limeidhinisha uteuzi wa mwakilishi wadi wa Tononoka Ali Omar Sharriff  kuwa mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji wa Umma na uhasibu.

Uteuzi huo unajiri baada ya nafasi hiyo kuachwa wazi na mwakilishi wadi wa Port Reiz  fadhil Mwalimu Makarani  ambaye pia ni naibu spika katika bunge la kaunti ya Mombasa aliyehudumu kwa miaka 3 kama mwenyekiti.

Hata hivyo Wawakilishi wadi wakiongozwa na Fadhil wamemtaja Shariff kama mchapa kazi na ambaye hana upendeleo.

Aidha Fadhil amemtakia heri katika nyadhfa yake hiyo akiamini kuwa ataendeleza gurudumu kama alivyokuwa wakati wake .

 

 

Kwa upande wake Ali  OmarSharriff ameahidi kushirikiana na wenzake katika kuhakikisha wanafanikiwa katimiza malengo huku akisisitiza kuwa wazi katika mambo yote anayoyafanya kwenye kamati hiyo.

Sharriff pia amewataka wakaazi wa Mombasa kutoa shaka kuhusu utumizi wa fedha za umma akiahidi kuzilinda na kutumiwa kutekeleza miradi ipasavyo.