Wanasiasa wa Isiolo walaumiwa kuchochea mzozo wa mpaka wa Eldera, Garissa County

Viongozi wa Kijamii maeneo ya kaskazini mwa Kenya walio katika kaunti ya Mombasa wamekashifu vikali matamshi ya baadhi ya viongozi wa eneo hilo kwa kile wanachodai ni uchochezi na matamshi ya kuzua uhasama.

 

Viongozi hao wanadai kuwa mwakilishi wa kike wa Isiolo Rehema Jaldesa pamoja na mbunge wa Isiolo kusini Abdi Kuropu wanachochea wakazi wa eneo la Eldera kuhusiana na mizozo ya mipaka inayoshuhudiwa sehemu hiyo.

Viongozi wa maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Kenya wakihutubia waandishi wa habari, Mombasa

 

Wakiongozwa na mwanaharakati wa kisiasa Abdul Qayum Sugow ameeleza kuwa licha ya eneo la Eldera ambalo limezua mzozo kuwa lipo katika kaunti ya Garissa, si jukumu la Wanasiasa kulijadili wala kuingilia kati ikizingatiwa kwamba mzozo huo umeibua mtafaruk na ghasia miongoni mwa wakazi.

AbdulQayum ameeleza kuwa ni jukumu la viongozi kuhubiri amani na wala sio kuwagawanya wananchi na akataka wakome mara moja na suala la mipaka waliachie waachie Tume huru ya uchaguzi na Mipaka, IEBC.

Kwa upande wake Sheikh Hassan Sugow ameongeza kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao hawana lengo la kuendeleza jamii bali kuwaganya hasa unapokaribia wakati wa uchaguzi, kwa kutoa matamshi ya migawanyiko na uchochezi.

 

Sugow sasa anaita idara ya usalama kupitia wizara ya usalama wa ndani kuingilia kati na kuwachukulia hatua viongozi wote wanaoendeleza chuki na siasa za miwawanyiko katika eneo hilo.

Haya yamejiri baada ya mzozo wa mpaka kuibuka katika eneo la Eldera linalozozaniwa kati ya kaunti ya Garissa na Isiolo.