Hatimaye Rais Evariste Ndayishime Awasili Kenya Siku kabla Ya Sherehe za Madaraka.

Photo Courtesy

Rais uhuru Kenyatta Amemkaribisha rasmi Rais wa Burundi Evariste Ndayishime akiwa pamoja na Mkewe Angeline Ndayubaha Ndayishime kwenye Ikulu ya Kisumu siku moja tu kabla ya maadhimisho ya sherehe za Madaraka hapo Kesho tarehe mosi Juni .

Aidha Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameuongoza ujumbe wa viongozi wakuu serikalini kumpokea Rais Ndayishime katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege mjini Kisumu ambapo Rais huyo wa Burundi atakuwa nchini kwa ziara ya siku 2.

Vile vile Rais huyo wa Burundi atafanyiwa mapokezi rasmi katika Ikulu Ndogo ya Kisumu kabla ya kufanyika kwa vikao na wajumbe nchini ambao utaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta hapo Kesho katika hafla ya Madaraka Dei.

Hata hivyo katika ziara yake nchini  Rais Evariste atapata fursa ya kuzuru miradi mbali mbali katika kaunti hio akiambatana na rais Uhuru Kenyatta Pamoja na viongozi wengine tajika nchini.