Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa aikashifu KeNHA kwa uzembe baada ya ajali iliyoua watu 15 barabara kuu ya Malindi-Msa

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa sasa anaitaka serikali kuu kumtia mbaroni mkandarasi ambaye amehusika katika ujenzi wa sehemu ya barabara eneo la  Kizingo katika barabara kuu ya Malindi kuelekea Mombasa kwa madai ya utepetevu. Hii ni baada ya  ajali iliyowaacha watu 15 kufariki na wengine kujeruhiwa katika sehemu hiyo.

Jumwa amesema  mhandisi huyo alikuwa mzembe na hakuweza kutekeleza majukumu yake vililivyo akidai kuwa ameiharibu barabara hyo badala ya kuijenga na kutaka ashtakiwe kwa makossa ya uuwaji.

Aidha Jumwa ameishtumu mamalaka ya kusimamia barabara kuu nchini KENHA kwa kuwa wazembe na kutowajibika vilivyo katika ukaguzi wa shughuli za ujenzi wa barabara.

Akiongea na wanahabari eneo la tukio Jumwa amesema  kutokana na kuchimbwa kwa barabara hiyo kumewapa madereva wakati mgumu haswa katika kupishana kutokana na ukosefu wa nafasi ya kutosha.

Jumwa ameahidi kushirikiana na familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo na kuiomba serkali ya kaunti ya Kilifi kusimamia shughuli zote za mazishi pamoja kulipia bili kwa walioko hospitalini.

Ajali hiyo imetokea eneo la Kwamkikuyu kwenye barabara kuu ya Malindi-Mombasa mapema leo,ikihusisha basi la kampuni ya Muhsin Bus lililokuwa safarini kwenda Garissa kutoka Mombasa na basi la kampuni ya Sabaki Shuttle lililokuwa likitoka Mombasa kwenda eneo la Merereni.

Madereva wote wawili walifariki papo hapo huku wafanyikazi sita wa kaunti ya kilifi wakiwa miongoni mwa walioaga katika ajali hiyo.