Rais Kenyatta atetea hatua ya kufunga kaunti 5

Rais Uhuru Kenyatta akihutubia taifa kutoka ikulu, Nairobi. Picha|PSCU

Rais Uhuru Kenyatta ametetea hatua yake ya kufunga mipaka za kaunti ya Nairobi,Kiambu,Machakos,Kajiado na Nakuru akisema uamuzi huo uliafikiwa baada ya mashauriano pevu na wadau na kuwa hatua hiyo ilikuwa ni ya kulinda wakenya.

“Najua kuna sekta mbalimbali kama za utalii na burudani yanayoumia. Hali ni ngumu lakini hatuwezi sema korona haipo.Njia ya kuokoa maisha ni kupitia hatua tulizoziweka,”akasema Rais Kenyatta.

Rais amesema hadi pale maambukizi yatapungua kwa asilimia 5 ndipo atakapotoa vikwazo alivyoviweka kwenye kaunti hizo.

kadhalika, rais Kenyatta amedokeza serikali kuu haipangi kuwapa wakenya kutoka kaunti hizo tano misaada ya fedha na rasilimali kwani vikwazo alivyoviweka ni vya mda tu wala haviathiri nchi nzima.

Vilevile,amewawakikishia wakenya waliopokea chanjo ya dosi ya kwanza kuwa hawatakosa ya pili.

“Tunafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunapata chanjo kwa muda mfupi unaohitajika.Nawahakikishia waliopata chanjo dosi ya  kwanza hawatokosa ya pili,”rais ameelezea.

Kwa upande mwingine, rais ametangaza kutoa msaada wa vifaa vya kidigitali vya kufanyia sensa 45,000 kwa nchi za Botswana,Sudan Kusini,Siera Lione,Namibia na Mauritius vitakavyowasaidia katika sensa.