Phillip Mpango ndiye makamu wa rais mpya wa Tanzania

Makamu wa rais mteule Dkt Phillip Mpango (Picha Kwa Hisani)

Bunge la Tanzania limeidhinisha  waziri wa fedha Dkt Philip Mpango kuchukuwa wadhfa wa makamu rais wa Tanzania baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu mapema leo.

Hadi kuteuliwa kwake, Dkt Mpango amekuwa waziri wa fedha na mipango tangu Novemba 2015.

Awali alihudumu kama kaimu kamishna wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru Tanzania TRA ,katibu mtendaji katika afisi ya rais akisimamia idara ya mipango kwa taifa hilo,Naibu katibu wa kudumu katika wizara ya fedha na uchumi na vilevile msaidizi  wa rais katika masuala ya uchumi.

Pia amewahi kuhudumu kama mkuu wa kitengo cha kushauri rais kuhusu uchumi,mtaalamu wa uchumi mkuu katika benki ya dunia na mhadhiri wa uchumi wa umma katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.