Abdulswamad aitaka kamati ya Kawi kutoa ripoti kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta nchini ndani ya siku 30

Mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir ametoa makataa ya siku 30 kwa kamati ya bunge la kitaifa inayohusika na masuala ya kawi kuwasilisha ripoti ya uchunguzi kuhusiana na suala la kupanda kwa bei  ya mafuta nchini.

Akizungumza wakati akiwasilisha hoja hio bungeni, Abdulswamad ameitaka kamati hiyo kufanya ripoti ya uchunguzi kwa mamlaka ya kawi nakuiomba kuwasilisha ripoti hio bungeni.

 

 

Abdulswamad amesema kupanda kwa bei ya bidhaa hio kumeathiri pakubwa ungezeko la bei za chakula,usafiri miongoni mwa bidhaa nyengine nchini.

Aidha amesema kuwa mamlaka hio imeshindwa na jukumu la kuwalinda wakenya akisema ongezeko la bei ya bidhaa hio iko juu ukilinganisha na mataifa mengine.

 

 

 

Ikumbukwe Suala hili linajiri siku chache  baada ya mamlaka ya kuthibiti kawi nchini kupandisha bei hio suala ambalo liliibua  hisia mseto miongoni mwa viongozi pamoja na wananchi.