Kina Mama Kwanza, Pinga Ugaidi na Itikadi Kali YOWPSUD Yabaini,Kisauni.

shirika linalojihusisha na udhibiti wa vurugu na itikadi kali miongoni mwa kina mama wachanga YOWPSUD limeanzisha mbinu ya kuwaeleimisha wakina mama  dhidi ya kujiingiza katika utumizi wa mihadarati  na itikadi kali

Katika kongamano lililowaleta pamoja kina mama  kutoka maeneo tofauti ya kaunti ya Mombasa liloandaliwa katika ukumbi wa freere town eneo bunge la nyali , afisa wa nyanjani wa YOWPSUD Muna Ismael  amesema wamekuwa wakiangazia sana maeneo ya Kisauni ,Bamburi na Shanzu.

Aidha Muna amesema hali ya uchochole hasa maeneo ya  kisauni ni sababu kubwa inayowafanya wakina mama kujiingiza kwenye makundi ya kihalifu ,na utumizi wa mihadarati hali inayovuruga usalama.

Wakati huo huo ,wakina mama hao wamelishukuru shirika hilo kwa juhudi zake za kuwaelemisha, wakisema manufaa wapatayo kutoka  kwa YOWPSUD  yatawasaidia katika jitihada zao za kukuza jamii bora ya badae.

kina mama wakipokea mafunzo ndani ya ukumbi wa freere town
mwandishi : Omar Mazera