Balozi wa Saudia Azuru Kituo Cha Radio Salaam Pamoja na Suleiman Shahbal

Balozi wa Saudia Arabia Mohammed A. Khayat amesifu juhudi wanazotia wanaandishi wa Habari kuwajuza na kuelimisha wananchi Habari mbali mbali katika kaunti ya Mombasa.

Ambassador Mohammed Khayat with Suleiman Shahbal, Salim A. Cheka and Preseter Omar and Judy

Balozi huyo ameyasema haya mapema hii leo alipoandamana na mfanyibiashara maarufu Suleiman Shahbal na kuzuru kituo chetu Radio Salaam katika eneo bunge la mvita jumba la Baluchi Complex hapa mjini Mombasa

Katika ziara fupi asubuhi ya leo Shahbal ambaye pia ni mgombea wa kiti cha ugavana Mwaka 2022 Pamoja na balozi Mohammed walipata fursa ya kutagamana na baadhi ya waandishi wa Habari katika kituo hicho  na kushuhudia shughuli za utayarishaji na upeperushaji wa vipindi, Habari na Matukio.

Aidha Mkurugenzi wa idhaa hii Salim Abdulrahman Cheka amepongeza hatua hio na kusema akuwa kama idhaa wamefarijika kutambulika na kutembelewa na balozi wa Saudia Pamoja na Shahbal huku akitoa changamoto kwa viongozi wengine kutambua vituo mbali mbali na juhudi wanazotekeleza waandishi wa Habari katika jamii .

Hata hivyo Balozi Mohammed ameahidi kushirikiana kwa kutoa msaada kwa wanaohitaji hasaa wakati jamii ya kiislam inakaribia mwezi mtukufu wa Ramadhan mwaka huu.

Mwandishi : Omar Khalfan