Abdulswamad aahidi makubwa mwaka 2022

Mbunge wa Mvita Abduswmad Sharif Nassir amewasuta viongozi wakisiasa  waliokuwa wakipinga ripoti ya BBI wakisema  kuwa haitapita na badala yake itaangushwa katika mabunge ya kaunti na sasa wakidai kuwa hawana shida yoyote na ripoti hyo baada ya kupita katika mabunge ya kaunti.

Akiongea katika mkutano wa Chama cha ODM ulioandaliwa eneo bunge la Likoni Abduswamad amewataja viongozi hao kuwa  walafi ambao wanataka kujifaidi wao badala ya wananchi waliowachagua.

Aidha amewaahidi wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuwa iwapo BBI itapita katika kura ya maamuzi na kuchaguliwa gavana mwaka 2022 atatumia asilimia 35 ya mgao atakaopata kufanya maendeleo zaidi ya wanayoyaona kwa sasa na kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na uongozi wake.

 

 

Aidha Abduswammad  amekosoa uamuzi wa baadhi ya viongozi wa Pwani  kuunda chama cha pwani wakati huu akihoji walikuwa wapi muda wote,na kuwataka kusimama na kumuunga mkono gavana wa Mombasa Hassan  Ali Joho ambaye tayari ameonyesha azma ya kugombania urais kupitia chama cha ODM akisema ni wakati wa Pwani kutoa kiongozi katika nyadhfa za juu.