Camels Joint nyumbani kwa vyakula murwa

Mji wa Mombasa nchini Kenya ni wa kihistoria. si kwa majengo yake bali lugha,mavazi na hata vyakula. Mombasa ni mji anaojizolea sifa si nchini tu bali

ulimwenguni kwa jumla kutokana na vyakula vyake vitamu ambavyo vimekuwepotangu kale.Hoteli nyingi Mjini Mombasa zimekuwa vivutio vikubwa kwa watalii hasa kwamahanjumati yao. Miongoni mwa hoteli zilizo na sifa ni hoteli ya Camels Joint .

Mwanzilishi wa Camels Joint ni Mzee Hasan  Saliim Swaleh Alamoody ambaye alianza kuuza juicena kisha kupiga hatua ya kufungua hoteli zaidi ya miaka 20 illiyopita. Camels joint ambayo kwa sasa ina matawi yake manne mjini Mombasa inapika karibia aina yote ya vyakula ulimwenguni jambo ambalo linawavutia watu kutoka kila pande ya dunia.

Umaarufu wa hoteli hiyo na biashara zake nzuri ndio sababu ya kupanuka kwahoteli hii na kuwa na matawi mbali mbali hivyo kutoa ajira kwa wingi hukuasilimia 75 ya walioajiriwa ni vijana.

Mohammed Khateeb ni msimamizi katika hoteli ya camels joint tawi la FortJESUS, anasema uwepo wa hoteli hiyo katika maeneo hayo ya kihistoria umewaletea wateja wengi hasa watalii kutoka nchi za ughaibuni.

 

Ujio wa ugonjwa wa corona umekuwa changamoto kubwa mojawapo ikiwa nikukosa wageni kutoka mataifa ya nje, kutokana na masharti yaliyowekwa na

serikali kudhibiti ugonjwa huo hasa marufuku ya kutoka nje usiku.

Aidha Khateeb anasema kuwa Camela joints inapania kupanua bishara yao kwa kufungua matawi zaidi nchini na kuboresha huduma zake kwa kuanzisha huduma za kupelekea watu vyakula majumbain ambao mwanzo mteja aaagiza chakula kupitia njia za kisasa za kimitandao vile vile watakuwa wkaitoa huduma za vyakula kwa sherehe za watu kuzaliwa na pia kutoa kumbi za kufanya mikutano.

 

 

Khateeb anawaaka wakaaji wapwani na wageni kuzidi kutembelea hotel ya camels joint ili kupata vyakula wavipendavyo na kwa huduma bora.

Ahmed Ali ni mmoja wa wateja wakubwa katika hoteli ya Camels joint na ana sifia mahanjumati yanayopikwa hapo.

“Mimi lazima nipitie Camelsjoint nile lunch kila siku labda niwe ni mgonjwa au nimesafiri, lakini kwa vyakula vinavyopikwa hapa na vilivyovitamu kamwe sitoacha kula Camelsjoint, maana chakulaukitakacho wakipata na kwa bei nafuu, mashalah Mungu awabariki” amesem Ahmed.

 

Iwapo utakuwa unahitaji sehemu ya kwenda kula mahanjumati ya kipwani basi Camels joint ndio pahala unapotakiwa kwenda

https://stootsou.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287