Supkem yamuomboleza Seneta Yusuf Haji

Baraza kuu la waislamu nchini Supkem limetuma risala za rambirambi kwa familia ya marehemu seneta Yusuf Hajj ambae ameaga dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Aga Khan jijini  Nairobi baada ya kuuguwa kwa muda.

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa Mwenyekiti  wa baraza hilo Ole Nado amemtaja marehemu kuwa kiongozi shupavu ,aliyekuwa na msimamo katika maswala ya kidini ,aliyependa amani na kuwashughulikia wanajamii haswa katika maswala ya elimu na maendeleo.

 

Aidha Nado amewarai viongozi na wakenya kwa jumla kudumisha amani wakati wanapoendelea kujadili swala la BBI ili kuwa na maisha yenye msingi bora kwa vizazi vijavyo na kama njia ya kumpa heshima mwenyekiti wa jopo la BBI marehemu Haji.

 

 

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza hilo tawi la Mombasa  Mukhdhar Khitamy amemtajata marehemu Haji kuwa kiongozi alietoa mchango mkubwa kwa umma na katika baraza hilo hadi lilipofikia na kusifia hatua zake za kupatanisha jamii kila sehemu alipohudumu  nchini ili kuleta amani. Marehemu Haji amekuwa mwakilishi wa wanachama wa kudumu katika baraza hilo,amefariki akiwa na umri wa miaka 80.