Said Twaha awarai vijana kuacha kutumiwa kisiasa

Mwanaharakati wa kisiasa Said Twaha amewarai vijana kuacha kutumiwa na wanasiasa ili kutimiza malengo yao badala yake kuungana na wale ambao watawawezesha katika shughuli zao za maisha.

 

 

Akiongea na wanahabari katika uzinduzi rasmi wa HUSTLER NA QUEENS katika eneo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa,Twaha ambaye amepanga kuwania ubunge wa Mvita mwaka 2022 amesema kuna baadhi ya mirengo ya kisiasa ambayo imekuwa ikiwahadaa vijana baada ya kuingia uongozini na kuwaomba kushikana na mrengo wa HUSTLER NATION ambao umekuwa ukiwawezesha vijana na kina mama katika katika shughuli zao za kila siku.

 

 

 

Kuhusiana na maswala ya ripoti ya BBI Twaha ameipinga vikali akisema haina manufaa yoyote kwa mwananchi wa kawaida bali kwa watu wachache. Twaha amesema bunge la Msa litashuritishwa kupitisha ripoti hiyo kwa kuwa limetawaliwa na viongozi waoga na wasioweza kutetea haki za wananchi waliowachagua.

 

 

 

 

Aidha Twaha amekashifu juhudi za baadhi ya viongozi wanaotaka kuwaunganisha wapwani akisema ni watu walio na agenda ya kujinufaisha wao wenyewe baada ya kushindwa kuwahudumikia wananchi wao kwa muda waliochaguliwa.

 

Said Twaha katika picha ya pamoja na vijana wa kundi la QUEENS FOR HUSTLER

 

Twaha amesema yeye na baadhi ya viongozi wa pwani wameamua kuungana na mrengo wa Ruto kwani ndio mrengo wenye suluhu la matatizo ya mkenya.