Mbunge wa Mvita aahidi kuendeleza vita dhidi ya mihadarati Kaunti ya Mombasa

Kumekuwa na changamoto nyingi katika jamii hususan katika suala la utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa jamii hapa nchini,huku ukanda wa pwani ukionekana kuathirika zaidi licha ya juhudi ya baadhi ya mashirika, viongozi wa kidini na kisiasa.

Akizungumza kwenye kikao na baadhi ya washikadau kutoka kwa mashirika mbali mbali ya kukabilina na mihadarati hapa Mombasa,mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesema kuna haja ya jamii kuhusishwa katika kukabiliana na vita dhidi ya utumizi wa mihadhati miongoni mwa jamii nchini.

Aidha dawa za kulevya hapa nchini zimeonekana kulemaza maendeleo katika jamii kutokana na kuwa vijana wengi wamejiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya.

Abdulswamad amesema tayari amepeleka mswada bungeni kuhusiana na utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa jamii hapa nchini.

Kulingana na ripoti ya utafiti ya mwaka 2010 nchini Kenya kuna waathiriwa wa dawa za kulevya 18,000 wanaotumia dawa hizo kwa njia ya kujidunga huku Mombasa ikiwa na idadi ya waathiriwa kati 8000 mpaka elfu 10,000, Idadi inayotajwa kuwa juu mno ukilinganisha na kaunti nyingine za ukanda wa Pwani.