Shirika La ndege la Boeing Kulipa fidia kwa waasiriwa wa ajali ya Boeing 737 Max

Ndege ya Boeing Picha kwa Hisani

Familia moja kutoka Kenya imepokea fidia ya takriban shilingi
milioni 300 kutoka Boeing juu ya ajali ya shirika la ndege la
Ethiopia.

Mnamo mwezi machi mwaka uliopita, takriban wakenya 32 ni
miongoni mwa abiria 149 walioangamia kwenye ajali ya ndege
aina ya Boeing 737 max iliyoanguka dakika sita tu baada ya
kupaa karibu na mji wa Bishoftu kusini-mashariki mwa uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Bole, Ethiopia.

Boeing 737 MAX ilipata ajali muda mfupi baada ya kupaa
angani kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole wa
Addis Ababa na kuwauwa watu 149.

Kando na taifa la Kenya kupoteza raia 32, Canada walipoteza
raia 18, Ethiopia 9, Italy 8, China 8, Marekani 8, Uingereza 7,
Wahindi 4, waslovakia 4 huku Ufaransa, Misri, Wajerumani
wakiwa na idadi 5 mtawalia.

Ribbeck Law Chartered, ambayo inawakilisha familia za
walioathiriwa kutokana na ajali hiyo ilielekea mahakamani
kudai dola bilioni 1 kama fidia kwa familia hizo.

Kesi hii ni ya kwanza kutatuliwa katika Mahakama ya shirikisho
la Amerika mjini Chicago dhidi ya Boeing kwa niaba ya familia
zilizoathirika.