Wabunge Nchini Kukatwa Mshahara Kulipia Marupurupu Haramu

Mahakama ya juu imeamrisha wabunge kurudisha sh 1.2 b waliojipatia kama marupurupu ya makaazi kwa njia isio ya kihalali.

karani wa bunge la kitaifa na baraza la seneti wamewamuru kupunguza pesa hizo kwa mishahara ya wabunge kwa kipindi cha miezi 12 ijayo.

Hukumu hio imetolewa Katika kikao kilicho hudhuriwa na majaji watatu akiwemo Pauline Nyamwenya, jaji Weldon Korir pamoja na jaji John Mativo.

Ikumbukwe kuwa Tume ya huduma ya bunge(PSC) iliwaongeza wabunge marupupu hayo ya 250,000 kila mwezi bila kufuatilia sheria za tume ya  kuratibu mishahara SRC na bila kujulisha tume hiyo mnamo mwaka 2018.

Wabunge  walikuwa wamepokea marupurupu hayo kwa miezi saba kwabla ya SRC kupata idhini ya koti kusimamisha malipo hayo.

Hii inamaanisha kwamba kila mbunge atahitajika kulipa shilingi  1.75m kwa muda wa miezi 12 kuanzia sasa.

Kesi hii iliwasilishwa mahakamani na tume ya SRC pamoja na mwanarakati Okiyo Omtata kwa madai kuwa wabunge walikuwa wakipokea marupurupu hayo mara mbili kwani yako kwa malipo yao ya jumla

Vile vile SRC wakiitaka tume ya PSC kutoingilia kazi yao suala lililoungwa mkono na mahakama na kuamua kwamba kazi ya mishahara iko mikonoi mwa SRC.

https://tobaltoyon.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287